top of page

Huduma Zinazotolewa

_DSC6150_edited.jpg

Huduma za utengemao kwa watoto wanaoishi na ulemavu.

Namba ya watoto waliosajiliwa mpaka sasa ni 615 na watu wazima ni 101.

​

Watoto wanaoishi na ulemavu wanapewa huduma za mazoezi tiba ya viungo na akili. Wazazi na wahudumu wanaoishi na watoto , wanafundishwa jinsi ya kuwatunza na jinsi ya kuwafanyia mazoezi kwa kuwashirikisha shughuli mbalimbali za kujimudu.

​Tunatoa huduma kwa wagonjwa wenye kiharusi, maumivu ya shingo,mgongo, viungo na misuli na pia kwa wale waliovunjika na wanahitaji mazoezi endelevu kwa muda

6.JPG

Huduma za utengemao kwenye jamii. / Vituo vidogovidogo.

Tunatoa huduma nyumba kwa nyumba kwa watoto wasioweza kufika kituoni kwa sababu za changamoto za kuichumi, kiumri na kimazingira.

​

Wataalam wanakutana na watoto katika vituo vidogovidogo vilivyopo kwenye jamii kwa ajili ya kuwafikia watoto walioko mbali na kituo kikuu.

8 A.jpeg

Mafundisho kwa wazazi na walezi./Mafundisho kwa serikari na jamii.

Tuna utaratibu wakutoa mafunzo kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kadiri ya aina ya ulemavu.
Tunatoa mafunzo kwa wenye viti na wasaidizi wao kuhusu sheria ya wenye ulemavu pamoja na wananchi kupitia mikutano yao.

_DSC6166.JPG

Huduma za lishe

Tunafanya utambuzi wa watoto wenye utapiamlo na kuwapa huduma za lishe kama vile maziwa, unga wa lishe na virutubishi, tunatoa elimu kwa wazazi na walezi namna ya kuandaa chakula cha lishe kwa mtoto na muda ambao wanapaswa kulishwa chakula

5.jpeg

Huduma za ushauri na saikolojia.

Tunatoa huduma ya utengemao kwa njia ya ushauri wa kisaikolojia kwa wazazi
na walezi wa watoto wenye ulemavu, kuwatia moyo kukubaliana na hali halisi za watoto wao. Vilevile tunawapatia ushauri wa kisheria kuhusu haki za mtoto mwenye ulemavu katika jamii.

8 B.jpeg

Huduma ya elimu jumuishi mashuleni

Tunashirikiana na walimu pamoja na wazazi kuingiza watoto wenye ulemavu mashuleni na kufuatilia maendeleo yao pamoja na kutoa elimu kwa walimu na wanafunzi kuhusu masuala ya watoto wenye ulemavu.

_DSC6051.JPG

Kutengeneza vifaa saidizi

Tunatengeneza vifaa saidizi mbalimbali kama vitu maalum (viti kona na viti choo), standing frame, magodoro na mito kwa mazoezi tiba n.k, kadiri ya mahitaji ya muhusika

Speech, occupational and cognitive therapy

Tukiongelea kuhusu ulemavu sio ulemavu wa viungo peke yake, lakini pia tunaangalia nyanja za mawasiliano na utambuzi.
Katika kituo chetu tunatoa huduma ya mawasiliano ili kuwasaidia watoto waweze kuimarika katika kuongea na kujenga mahusiano mazuri na wengine. 

bottom of page